Faida za kuwa na blogu

Faida za kuwa na blogu ni nyingi kwa wale ambao wana tafuta njia mbadala ya kufikisha ujembe wao kwa haraka, urahisi na unafuu. Baadhi ya faidi kubwa za kuwa na blogu ni; Blogu ni rahisi kuanzisha na kusimamia; 
Kuanzisha blogu ni rahisi sana na inachukua chini ya dakika 5 kuanzisha blogu yako bila gharama yeyote zaidi ya kuwa na mtandao. Vile vile kuendesha na kusimamia blogu yako ni rahisi kwani unaweza kuweka makala zako mtandaoni kwa kutumia simu, barua pepe n.k. 


 Ni rafiki wa search engine; Zaidi ya nusu ya watu wote wanaotumia mtandao duniani hutumia search engines kutafuta makala mtandaoni. Ukiweza kutumia blogu yako vizuri unaweza kufaidika na utitiri wa watu wanaotumia search engines. Blogu tofauti na tovuti zingine inauwezo mkubwa wa kufaidika na search engine ambayo itakuletea wageni wengi ukiitumia vizuri. 

 Blogu huvuta wageni wengi; Uwezo mkubwa wa kutumia search engines, uhamasishaji wa ushiriki kwa kutoa maoni unasaidia blogu kuvutia watu wengi kuliko tovuti nyingine. Ukiweza kuweka makala zenye mvuti, zenye kuhabarisha, kuelimisha, kuburudisha n.k. hutakosa wageni kwenye Blogu yako mfano Blogu ya Issa Michuzi, ni maarufu si kwa sababu ya Michuzi bali ni kwa sababu ya maudhui yake.

 Blogu itakupatia kipato; Ukiweza kuwa na maudhui yenye mzuti, ukatumia search engine vizuri utapata wageni wengi kwenye blogu yako. Ukiwa na watu wengi wanaotembelea blogu yako, watu, makampuni nakadhalika watataka kuwafikia wageni wanaotembelea blogu yako. Njia ya kuwafikia ni matangazo ambayo itabidi wakulipe hivyo kukuingia kipato. 

 Blogu inaweza kukupatia ajira; Kwa wale ambao hawana ajira na wanaujuzi fulani au wamesomea kitu Fulani, blogu inaweza kuwa njia ya kukupatia ajira. Mfano umesomea ubunifu wa majengo na huna ajira unaweza kuanzisha blogu ambayo inatoa ushauri kuhusu namna bora ya ujenzi bure. 

Endelea kupata huduma zetu zenye ubora.

Post a Comment

0 Comments